Hongera kwa kuianza safari hii ambayo itabadilisha mawazo yako na mtazamo wako na kukufanya utumie muda wako wa ziada kujinufaisha na hata kubadilisha maisha yako kabisa.
Haijalishi unafanya kazi gani, umesomea fani gani au una level gani ya elimu, unaweza kutumia fani uliyonayo kujiongezea kipato kupitia blog au website. pia unaweza kuwashirikisha wenzako kitu unachokipenda kupitia blog au website na ukajiajiri kupitia hicho kitu na kujiongezea pesa.
Haijalishi unafanya kazi gani, umesomea fani gani au una level gani ya elimu, unaweza kutumia fani uliyonayo kujiongezea kipato kupitia blog au website. pia unaweza kuwashirikisha wenzako kitu unachokipenda kupitia blog au website na ukajiajiri kupitia hicho kitu na kujiongezea pesa.
HAWA NI BAADHI YA WATU AMBAO WAMETAJIRIKA KUPITIA BLOGS NA WEBSITE NA HATA KUACHA KAZI WALIZOKUWA WAKIFANYA KABLA YA HAPO
Usijali kuhusu adsense, adsense ni njia ya kutangaza blog yako ambapo google watakutangazia blog yako kwenye site za wengine ili upate visitors wa kutosha kwenyenye blog au website yako, japo utalipia lakin hela yako itarudi ndani ya siku chache. na ukishapata visitors wengi google wataweka matangazo kwenye site yako na utaanza kulipwa kwa kila tangazo.
JE UNAWEZAJE KUPATA PESA AU KULIPWA KUPITIA BLOG?
1: Mwanzoni kabisa nimekuambia kuwa kuna kitu kinaitwa Adsense na nikakuambia kuwa adsense ni matangazo ambayo google wanayaweka kwenye blog au website yako kwa. google watakulipa pale watu watakavyoingia kwenye blog yako na kusoma au kufungua matangazo yao waliyoyaweka.
Hivyo ili uwezwe kulipwa au kunufaika kupitia online ni lazima uwe unapata visitors(watu watakaoingia kwanye blog yako) na wawe wengi. kadri watu watakavyokuwa wengi ndivyo utakavyolipwa hela nyingi hivyo ni jitihada zako kuhakikisha unapata watu wa kutosha.
Usihofu kuhusu hilo kwani unaweza kutumia mitandao ya kijamii kama facebook, twitter, instagram na mingineyo mingi kujitangaza na kupata watu wa kutosha.
2: Pia kampuni, mashirika kama vile CRDB au NMB na mengineyo au mtu binafsi anaweza akatangaza biashara yake, au kampuni yake kwenye blog yako na akakulipa kiasi fulani cha pesa.
3: Pia wewe binafsi unaweza kuitumia blog au website yako kutangazia biashara zako ambapo unaweza ukajiongezea wateja na pia kuwafikia wateja walioko mbali na eneo unalofanyia biashara yako kiurahisi na kwa gharama nafuu.
UNACHOHITAJI:
Uwezo wa kusoma na kuandika, uwe na simu, computer au desktop. pia huitaji kuwa na uzoefu wala ujuzi kuhusu wabsite na blogs. huitaji kuwa na wafuasi(followers) wengi (japo nitakuelekeza namna ya kuwapata kupitia mitandao mbalimbali ya kijamii.
kwenye hii post sikufundishi namna ya kutengeneza website au blog japo nitakufundisha kwenye post zijazo.
ILI KUANZA SAFARI YAKO YA KUJITENGENEZEA PESA ONLINE UNAHITAJI KUFANYA YAFUATAYO.
1:Kujiamini, usihofie labda kwa kuwa ni jambo geni kwako.
Amini kuwa unaweza kuwa na website au blog na kuifanyia jambo lolote ambalo unahisi kuwa ni zuri na linapendwa na pia linaweza likaisaidia jamii iwe ni kuburudisha, kufahamisha au kuelimisha jamii. ninasema kujiamini kwa sababu watu wengi wamekuwa wakihisi kama ni vile kuwa na blog au website ni jambo zito ambalo labda linahitaji uwe umesomea au una uzoefu katika fani ya IT aumpaka wawe na hela nyingi kwa ajili ya kumlipa mtaalamu ili amtengenezee. kama wewe ni miongoni mwa watu waliokuwa wakiwa na fikra kama hizo basi ondoa hiyo hofu maana ninaenda kukusaidia. ukishatoa uoga ulionao waweza kufanya yafuatayo.
2: Tengeneneza marafiki, wafuasi wa blog yako (FOLLOWERS)
Kama una ndoto za kutengeneza hela kupitia blog au website basi unahitaji kwanza ujihakikishie marafiki wafuasi(followers) wengi kadri uwezavyo. wengine tayari mna zaid ya 500 Twitter, instagram na facebook followers. lakini bado unahitaji kuwaongeza na kuwa na followers wengi kadri uwezavyo. cha kufanya kwa sasa ni kujiunga na mitandao ya kijamii kama vile twitter, instagram, facebook na mingiyo mingi. kama tayari una marafiki(followers) wa kutosha basi upo kwenye hatua nzuri ya kuanza kuujaza mfuko wako.
3: Post mambo ambayo watu watayapenda ili wakufollow(post things that people will attract people to view your blog or website)
Baada ya kujiunga na mitandao ya kijamii hakikisha unapata wafuasi wengi kwa kutuma jumbe zitakazowanya wakuadd kama rafiki au kukufollow na pia hakikisha unatuma ujumbe ambao utawafanya waendelee kuangalia page yako mara kwa mara. kumbuka kuwa wao ndio watakaokuingizia kipato baadae. hivyo ni vyema ukatumia lugha ya upole pale unapotuma kitu. ukishajihakikishia wafuasi/marafiki(followers) wa kutosha utahitaji kufanya kifuatacho.
4: Tafuta au fikiria jina zuri la website au blog yako unayoenda kuitengeneza au kutengenezewa.
Mfano unitchno.com, example.com, name.com. usichukue muda mwingi kuchagua jina la site yako kwasababu kitakachokuletea watu kwenye website yako ni huduma unayotoa au kilichopo kwenye website yako ambacho kitawavutia watu waingie kwenye site yako.(Note the content of your site is much more important than your domain name).
5: Nunua domain name au unaweza kutumia free domain names
Je ni nini maana ya Domain name?
domain name ni jina la blog au website yako ambalo mfano ni kama example.com, wewe.com au shule.com inategemea na unavyopenda wewe.
Je ni kwanini ununue domain name?
kununua domain name ni bora zaid kwa sababu unakuwa free kufanya mambo yako bila mwingiliano na unakuwa na uwanja mpana zaid kwa ajili ya kufanya mambo yako (hakuna masharti). unaweza kupata free domain kwenye hii link www.weebly.com au kununua kupitia www.ecowebhosting.co.uk.
Je utawezaje kuwa na blog yako?.
Je unadhani ni kazi ngumu sana kuwa na blog au website?.
Je unahitaji kuwa na kiasi kikubwa cha pesa ili kuwa na website au blog?
Jibu ni hapana, cha kufanya endelea kufuatilia post zangu, soon nitakufundisha hatua kwa hatua, lakini kama unahitaji nikutengenezee tafadhali usichelewe kunitafuta kupitia anuani zangu au namba ya simu niliyoiweka hapo chini.